Embu: Waziri Matiang'i Aitembelea Familia ya Kaka 2 Waliouawa Mikononi mwa Polisi
- Benson Njiru Ndwiga na Emmanuel Mutura walipatikana wameuawa kwa njia tatanishi baada ya kukamatwa na polisi kwa kuvunja sheria za kafyu
- Mauaji ya kaka hao wawili yalisababisha maandamano makali eneo la Kianjokoma mjini Embu ambapo mtu mmoja alipoteza maisha yake
- Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i aliitembelea familia Jumatano, Agosti 11, na kuihakikishia kwamba haki itatendeka
- Wawili hao wanatarajiwa kuzikwa Ijumaa, Agosti 13 nyumbani kwa baba yao kaunti ya Embu
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i siku ya Jumatano, Agosti 11, aliitembelea familia ya kaka wawili waliouawa kinyama wakiwa mikononi mwa polisi kaunti ya Embu Agosti Mosi.
Benson Njiru Ndwiga na Emmanuel Mutura walipatikana wameuawa kwa njia tatanishi baada ya kukamatwa kwa kuvunja sheria za kafyu.
Akizungumza na waandishi wa habari saa chache baada ya kukutana na familia ya wendazao, Matiang'i alisema ameahidi familia kwamba haki itatendeka pindi uchunguzi utakapokamilika.
" Mashirika husika yanafanya uchunguzi, kitengo chetu cha usalama wa ndani kikishirikana shirika la IPOA kishaanzisha uchunguzi. Nimekutana na baba wa wavulana hao nikiwa na mwanasheria mkuu na inspekta jenerali wa polisi, tutafanya kila kitu kadri ya uwezo wetu ili haki itendeke kwa familia," Matiang'i alisema.
Kaka 2 Waliouawa Embu Mikononi mwa Polisi Walikuwa Wameanzisha Biashara ya Nguruwe
Kulingana na Waziri Matiang'i uchunguzi unaendelea vema na ana matumaini kwamba chanzo cha vifo vya wawili hao kitabainika hivi karibuni.
Matiang'i pia alisema Wizara yake haitalala hadi haki ipatikane kwa wavulana hao ambao vifo vyao vimekuwa pigo kubwa kwa jamaa na familia kwa jumla.
" Kazi nyingi tayari imefanywa, sitaki kuzungumzia yale yanaenda kutendeka. Nimearifiwa kwamba uchunguzi unaendelea vizuri na sisis kma watumishi wa umma, tumefanya mazungumzo na baba ya wavulana hao na tumemuhakikishia kwamba tutafanya jinsi sisi hufanya ila kulingana na sheria," Aliongezea Matiang'i.
Mauaji ya kaka hao wawili yalisababisha maandamano makali eneo la Kianjokoma mjini Embu ambapo mtu mmoja alipoteza maisha yake.
Kulingana na shahidi aliyezungumza na wanahabari, Ndwiga na Mutura walifikishwa katika kituo cha polisi cha Manyatta wakiwa na washukiwa wengine lakini wao hawakushukishwa kutoka kwenye gari.
Dakika chache baadaye, polisi wawili wanasemekana kuondoka na wawili hao wasijue walikokuwa wakielekea.
Polisi hao baadaye walidai kwamba Ndwiga na Njiru waliruka kutoka kwa gari lao lililokuwa likiendeshwa kwa kasi.
Bweni la Shule ya Upili ya St. Bridgit's, Kiminini Lateketea, Chanzo cha Moto Hakijabainika
Hata hivyo, shahidi mwingine ambaye alikuwa tayari ameandikisha taarifa kwa polisi, alisema Mutura, 19 ndiye alikuwa wa kwanza kukamatwa.
Shahidi huyo alisema maafisa wa polisi walianza kumpiga na alipoona hivyo, kakake Ndwiga alijaribu kumuokoa lakini pia alinyamazishwa kwa kupigwa.
" Walimpiga kwenye kichwa na alikuwa amelala chini akiwa amepoteza fahamu, afisa mwingine alimpiga Ndwiga alipojaribu kumuokoa kakake, naye pia alianguka chini, ilionekana ni kana kwamba walitaka kumzima kwa sababu alikuwa ameona kakake akipigwa bila huruma," Alisema shahidi.
Baada ya kuchapwa, wawili hao waliwekwa kwenye viti vya mbele ndani ya gari la polisi hao na wakaelekea katika kituo cha polisi cha Manyatta, gari hilo liliegeshwa nje ya seli, washukiwa wengine waliamurishwa kushuka lakini kaka hao walisalia ndani ya gari.
Haikubainika kilichotendeka baadaye lakini saa chache baada ya ripoti ya vifo vya wawili hao kutangazwa, ilisemakana kwamba waliruka nje ya gari walipokuwa wakipelekwa kituoni.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Nakuru: Watu 5 Wafariki Dunia Baada ya Kushukiwa Kunywa Chang’aa Yenye Sumu
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ39zfJFmnKaapWLEosbIq6BmpZGptqK6xqJkmqGkmrqjscuemGaekaK2rbXAZrCaZZuWuKJ5kWaumqSZpMKiw8BmpKKjn6O8r7WMpq6aZaCkuaq%2FyGefraWc