Kamati ya Mazishi: Moses Kuria Awatania Maina Kamanda na Wenzake Baada ya Kukutana na Raila

Publish date: 2024-09-02

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria angali anasherekea ushindi wa wagombea aliokuwa akiunga mkono Kiambaa na Juja kwenye chaguzi ndogo za Mei na Julai.

Kuria alisema Jubilee ilimalizwa wakati wa uchaguzi mdogo Juja Mei 18 na kilichokuwa kikisubiriwa kule Kiambaa ni mazishi tu.

Ushindi wa Kiambaa Julai 15 ulimfanya kupuuza viongozi wanaoegemea upande wa Rais Uhuru Kenyatta ambao walikuwa wakiongoza kampeni za Kiambaa kama 'kamati ya mazishi'.

Viongozi hao wakiongozwa na Maina Kamanda, Amos Kimunya, Peter Mwathi na Kanini Kega walikuwa Mombasa Jumatano Julai 21 ambapo walikutana na kinara wa ODM Raila Odinga.

Pia soma

Raila Odinga Akutana na Wabunge wa Mlima Kenya, Wanamtandao Wasema Anachezwa

Habari Nyingine: Askari Jela Akamatwa kufuatia Tuhuma za Visa vya Utekaji Nyara

Kupitia kwa mtandao wake wa Facebook, Kuria alisema kilichokuwa kikiendelea kwenye kikao cha viongozi hao na Raila ni mipango ya mwisho ya 'kamati ya mazishi'.

"Mkutano wa mwisho wa kuvunja kamati ya mazishi ya Jubilee," alisema mbunge huyo matata.

Chama cha Kuria cha Peoples Empowerment Party (PEP) ndicho kiliipa Jubilee kichapo baada ya mgombea wake George Koimburi kumshinda Susan Wakapee wa Jubilee.

Habari Nyingine: Picha ya Mbwa Waliohudhuria Mazishi na Kuomboleza Yazua Mdahalo

Wandani wa DP, akiwamo Kuria, wamekuwa wakishikilia kuwa kurambishwa sakafu kwa Jubilee katika uchaguzi huo mdogo wa Kiambaa ni ishara ya kusambaratika na kuanguka.

Mgombea kinda wa chama cha UDA kinachohusishwa na naibu rais WIlliam Ruto Njuguna Wanjiku ndiye alimbwaga Kariri Njama wa Jubilee.

Njuguna alizoa kura 21,773 akifuatwa kwa karibu sana na Kariri, aliyepata 21,263 kwenye uchaguzi huo wa Julai 15.

Pia soma

Mbunge Mtarajiwa wa Kiambaa Aelezea Alivyotekwa Nyara na Kuvuliwa Nguo

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoZ3fJRmopqlkam2bsXAZqSaspmotap5zKiqnqtdoMKztcBmmLCZpJa7qq2MppiippFiuKK5wKebmmWelnq4sc2zmKSdXZeuorDAZrCaZZuquLbAwKeYZqaRYr%2BitcuaZaGsnaE%3D