Wabunge 16 Wafurahia Minofu Dubai Wakenya Wakilala Njaa

Publish date: 2024-07-27

- Huku Wakenya wakilia kuhusu gharama ya maisha na kuongezeka kwa mzigo wa kiuchumi, viongozi wao walisafiri Dubai ambapo watatumia mamilioni

- Wakenya wanahisi serikali inaendelea kutumia ushuru ambao unaokotwa vibaya bila kujali walala hoi

- Wabunge waliohudhuria kikao hicho walisema ni muhimu ili kuwezesha kupiga msasa matumizi ya fedha za umma

Wakenya wamekerwa na hatua ya wabunge 16 kusafiri nchini Dubai kuhudhuria hafla ya kujifunza kuhusu matumizi bora ya fedha za umma.

Kundi hilo la wabunge liliondoka nchini siku ya Alhamisi wiki jana na wanatarajiwa kurejea Jumamosi Machi 20.

Ziara hiyo imejiri wakati ambapo Wakenya wanakatwa maini na makali ya janga la coronavirus baada ya uchumi kuharibika.

Aidha gharama ya maisha inazidi kupanda na iliwachoma roho sana walipa ushuru kuwa wabunge hao watapokeo mamilioni kutoka kwa mfuko wa mlipa ushuru kama marupurupu.

Habari Nyingine: Uhuru Mtaani: Picha ya Rais Jijini Bila Walinda Usalama Yaibuka Mtandaoni

Gazeti la Standard liliripoti kuwa wabunge hao wataenda nyumbani na takriban KSh 20M huku kila mmoja akitia mfukoni KSh 1.28M.

Wabunge hao ni kutoka kamati za bunge zinazohusiana na masuala ya fedha na wanajumuisha Mbunge wa Nyali Mohammed Ali pamoja na mwakilishi wa kinana kaunti ya Nairobi Esther Passaris.

Ali, maarufu kama Jicho Pevu, alitetea ziara hiyo akisema ni muhimu katika kuhakikisha matumizi mazuri ya fedha za umma.

Habari Nyingine: Magazeti Jumatano: Rais Uhuru Awazomea Vigogo wa NASA na Kuwataka Kuungana

"Hii ni ziara iliyolipiwa na serikali na ilipangwa miezi mingi iliyopita na madhumuni yake nu kuwezesha wabunge waweze kupiga msasa matumizi ya fedha za umma," alisema Jicho Pevu.

Gharama ya maisha imekuwa ikipanda na kwa sasa Wakenya wamekuwa wakilia kuhusu kuongezeka kwa ushuru unaokatwa na serikali.

Kumekuwa na maswali kuhusu jinsi fedha hizo zinatumika baada ya kuokotwa huku wengi wakihisi zinafunjwa na viongozi serikali.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZYNxfpRmrpqapaO0pnmQb2SwmZaqv6K0yJpkpqGepLO2ecOumZqhXayurLHNsphmr5Ggtq2ty5pkp6KRlnupwMyl