Spika Justin Muturi atawazwa msemaji wa jamii ya Mlima Kenya

Publish date: 2024-08-19

- Muturi alitawazwa msemaji wa Mt Kenya na wazee wa Njuri Ncheke Jumamosi Machi 6

- Eneo la Mlima limekuwa katika harakati zakumtafuta mrithi wa Rais Uhuru akiondoka 2022

- Wanasiasa kadhaa wamekuwa wakijaribu kujipanga ili kuchukua nafasi hiyo

Spika wa bunge Justin Muturi ametawazwa kama msemaji wa jamii ya Mlima Kenya huku siasa za urithi wa uongozi wa eneo hilo zikiendelea kushika kasi.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kustaafu kutoka siasa 2022 na eneo hilo linamtafuta atakayechukua viatu vyake.

Hafla ya kumfanya Muturi msemaji wa Mt Kenya ilifantyika Jumamosi Machi 6 katika ,ojawapo wa maeneo takatifu ya wazee wa njuri Ncheke huko Tigania.

Ni hafla ambayo ilihudhuriwa na mami ya wazee kutoka Mt Kenya wakiwemo wandani wa Rais Uhuru.

Habari Nyingine: Nakuru: Watu sita waangamia kwenye ajali ya barabara Njoro

Mwenyekiti wa Njuri Ncheke Josphat Murangiri alisema hafla hiyo ni muhimu sana kwani eneo la Mt Kenya litabaki bila kigogo baada ya Rais kuondoka.

"Muturi ni mwanasiasa mkuu kutoka eneo la Mlima Kenya na tunataka sauti yetu kuskika,"Murangiri alisema.

Kulingana na historia ya wazee hao, Muturi ni watano kutawazwa kiongozi tangu uhuru na anaingia orodha ya Jomo Kenyatta, aliyekuwa rais Mwai Kibaki, Uhuru, na Gavana wa Meru Kiraitu Murungi.

Habari Nyingine: Kahawa West: Kijogoo akanyaga kinyesi akihepa kichapo cha sponsa

Eneo la Mlima limekuwa likitafuta atakayekuwa jogoo baada ya Rais kumaliza kipindi chake afisini na viongozi kama vile magavana Mwangi wa Iria (Murang'a), Anne Waiguru (Kirinyaga), Waziri Peter Munya, Mbunge Moses Kuria na aliyekuwa waziri Mwangi Kiunjuri wanamezea mate wadhifa huo.

Muturi amekuwa mmoja wa wandani wa Rais Uhuru tangu wakiwa wachanga na anahudumu kipindi chake cha pili kama spika wa bunge.

Naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe alisema Rais atasalia kigogo wa Mt Kenya hata baada ya kuondoka mamlakani 2022.

Akiongea awali alipokutana na MCAs kutoka Mlima Kenya kuwarais kupigia kura BBI, Rais pia alisisitiza ni lazima atakuwa kwenye meza ya kujadili uongozi wa Mt Kenya baada ya 2022.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZYF6g5Bmqqmhm5Z6q8HSraCnZZ2qwba%2ByGaYrZmnlse4rYymqp6lkZ%2B2bsPAZqGapZmeerqtjKajoqWRYrimutiaZaGsnaE%3D