COVID -19: Watu 394 wapata coronavirus, 10 wapoteza maisha yao

Publish date: 2024-09-16

- Taarifa kutoka Wizara ya Afya ilionesha jumla ya wagonjwa nchini imefika 92,852

- Wagonjwa 271 ni wanaume nao 123 ni wanawake

- Wagonjwa 810 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini

Kenya imeandikisha visa vingine 394 vya coronavirus baada ya sampuli 5,752 kupimwa katika saa 24 zilizopita.

Taarifa kutoka kwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe mnamo Jumatano, Disemba 16 ilisema kwamba jumla ya wagonjwa nchini imegonga 92,852.

Habari Nyingine: Aliyekuwa ripota wa NTV mashinani achaguliwa MCA

Kuhusu jinsia wagonjwa 271 ni wanaume nao 123 ni wanawake huku mgonjwa mwenye umri wa chini akiwa na miaka mitatu na mkongwe zaidi miaka 93.

Aidha wagonjwa 424 wamepata nafuu ambapo 303 walikuwa wanauguzwa nyumbani nao 121 kutoka hospitali mbali mbali nchini.

Habari Nyingine: Barobaro aachwa mataani na demu

Aidha, idadi ya wagonjwa waliopata nafuu nchini imefika 74,403

Wakati uo huo, wagonjwa 10 walifariki dunia kutokana na makali ya virusi hivyo ambapo sasa idadi ya walioangamizwa imefika 1,614.

Habari Nyingine: Abiria afariki dunia akiwa ameketi kwenye kiti ndani ya basi

Kufikia sasa wagonjwa 810 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini na 6,172 wanapokea huduma za kimatibabu wakiwa manyumbani mwao.

Wagonjwa 46 nao wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Habari Nyingine: Aliyekuwa seneta wa Machakos Muthama aachiliwa kwa dhamana ya KSh 30K

Maambukizi mapya yalirekodiwa kama ifuatavyo ; Nairobi 167, Mombasa 59, Taita Taveta 32, Kwale 21, Kilifi 20, Nyeri 13, Kiambu 12, Nandi 7, Kakamega 7 , Siaya 6 , Kajiado 6 , Bungoma 6.

Nakuru 5 , Meru 5 , Nyamira 5 , Migori 5 , Kisii 4 , Kisumu 3, Turkana 2 , Murang'a 2 , Machakos 2 , Narok 1 , Mandera 1, Vihiga 1 , Homa Bay 1 , na Lamu 1.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Soma taarifa zaidi kwa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjboN6gZhmmqiumZl6bn2YZq6arKVigHqAjLCYqZmklnqku9GopZqumafCtHmQaWSwmaCkwabGwGakmqGjna5uxcCoZaGsnaE%3D