Miili ya watu 10 waliozama Ziwani Victoria yaopolewa yote
- Boti iliyokuwa imewabeba wabiria 20 kutoka Uganda ikielekea Usenge, Siaya ilizama Ziwani Victoria na kusababisha vifo vya watu 10
- 10 waliokolewa na wavuvi waliokuwa eneo la mkasa
- Siku mbili baada ya watu 10 waliopoteza maisha baada ya kuzama imeopolewa yote
Kamanda Mkuu wa polisi mkoani Nyanza Karanja Muiruri amethibitisha kwamba miili ya watu 10 waliozama katika Ziwa Victoria Jumanne, Novemba 17 imeopolewa yote.
Akizungumza na vyombo vya habari,, Ijumaa, Novemba 20, Muiruri alisema tayari kila familia imepokea mwili wa mpendwa wao kwa ajili ya kujiandaa kwa mazishi.
Habari Nyingine: Waziri Kagwe anawazia kuharibu michuzi ya Krisimasi, kisa Covid-19
Habari Nyingine: Madaktari waanza mgomo kaunti ya Bomet, washinikiza nyongeza ya mishahara
Muiruri ameongezea kwamba maafisa wa Kenya Coast Guards ndio waliofanikisha shughuli hiyo ya uopoaji.
Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, boti hiyo ambayo ilikuwa imebeba abiria 20 ilizama baada ya kupigwa na upepo mkali.
Kamishna wa kaunti ya Siaya Francis Kooli pia alisema boti hiyo ambayo ilikuwa inatokea nchini Uganda ulikuwa imebeba mizigo ikiwemo mahindi na ilikuwa inaelekea Usenge.
Habari Nyingine: Mwanamke anayedai kuwa mpenzi wa mbunge Justus Murunga aende kortini kuzuia mazishi yake
Watu kumi walizama maji huku 10 wakiokolewa na wavuvi waliokuwa eneo la mkasa wakivua samaki.
Wakenya mitandaoni na viongozi kadhaa akiwemo Naibu Rais William Ruto waliomboleza vifo vya 10 hao.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Ruto aliandika, "Ni habari za kuhuzunisha kusikia kwamba tumewapoteza watu 10 waliozama katika Ziwa Victoria. Ningependa kutuma risala zangu za rambi rambi kwa familia zilizoathirika na mkasa huo, Mungu na azidi kuzipa nguvu wakati huu wa majonzi."
Hii sio mara ya kwanza mkasa wa boti kutokea katika Ziwa Victoria, mnamo Mei 2020, feri ambayo ilikuwa imebeba watu 17 ilizama.
Feri hiyo ilidaiwa kupigwa na mawimbi makali na ilikubwa na hitilafu, habari njema ni kwamba abiria wote waliokolewa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari zaidi kutoka hapa TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdjbn9yg5RmpKKhnJ56uq2MsJitrV1mfW7DwKWgqLKRoq5uxsiwmKehXau2pMDOq6CaZamWvLG7y56ummWppMGmesetpKU%3D