Magazeti ya Jumanne, Mei 26: Macho yote kwa DP Ruto wakati wa mkutano wa Uhuru Ikulu

Publish date: 2024-09-02

Huku kufunguliwa kwa uchumi ukiendelea kushinikizwa, magazeti ya Jumanne, Mei 26, yanaripoti kuwa viongozi kadha wamejitokeza na kutoa ushauri kwa kile wanaona ni njia bora katika kulinda maisha na kuendelea kupata mapato.

Magazeti haya pia yanatathmini mpasuko kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto na kujaribu kuonyesha kwamba wawili hao wanakinzana.

Habari Nyingine: Mbunge Babu Owino akwaruzana na mtangazaji Anne Kiguta wakati wa mahojiano

Habari Nyingine: Mchezaji wa Cameroon, Joseph Bouasse aaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo

1. People Daily

Makamu wa Rais William Ruto ameelezewa kama mwanamume ambaye anaingia katika historia kama naibu wa rais pekee anayeshikilia mamlaka kubwa kinyume na wenzake 10 waliomtangulia.

Hata hivyo, kulingana na People Daily, Rais Uhuru Kenyatta aliamua kumuachia Ruto mamlaka kubwa wakati wa hatamu yao ya kwanza (2013-2017) ili kumsaidia kuchagulia tena kwa muhula wa pili.

Haya yalinakiliwa vibaya na Ruto na wandani wake ambao walidhania wawili hao wana mamlaka sawa.

Baada ya kuchaguliwa kwa mara ya pili, gazeti hili linasema kuwa Uhuru alibadilisha msimamo wake kwa kumpunguzia Ruto mamlaka na ushawishi na hivyo kumtupa nje kwa baridi pamoja na washirika wake.

2. Taifa Leo

Taifa Leo linaripoti kuwa Rais Uhuru anatumia janga la sasa la virusi vya corona kumuadhibu naibu wake William Ruto.

Ghafla baada ya kisa cha kwanza kuripotiwa nchini, Uhuru alipiga marufuku mikutano ya hadhara ikiwemo ya makanisa ambapo Ruto na wandani wake walitumia kupigia debe ajenda yao na kukashifu serikali.

Ni wakati huo ambapo Uhuru, ambaye ndiye kiongozi wa Chama cha Jubilee, alifanyia mabadiliko Kamati ya Taifa kwa kuwateua wanachama wapya.

Naibu Rais na kambi yake walipinga hatua hiyo lakini Rais aliwapuuza.

Kiongozi wa Raifa pia aliwaondoa washirika wa Ruto kutoka kwa nyadhifa za naibu spika Seneti Kiongozi wa Wengi Seneti na Kiranja wa Wengi Seneti na kuwaweka washirika wake wakati huu wa janga.

Mchakato huo sasa unalenga Bunge la Taifa na kamati za bunge huku wandani wa Ruto wakionekana kuweka roho mkononi.

Uhuru pia anapania kuandaa mkutano na Kamati la Kundi ya Bunge katika nia ya kuwapiga teke wanachama wakaidi wakati ambapo mkusanyiko wa watu zaidi ya 15 ulipigwa marufuku kuzuia kuenea kwa COVID-19.

3. The Star

Naibu Rais William Ruto ndiye mtu wa kuhofiwa sana wakati wa misururu ya mikutano itakayoandaliwa na Rais Uhuru kujadili masuala ya Chama cha Jubilee.

Uhuru anatazamiwa kukutana na wanachama wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa Chama cha Jubilee (NMC), ambao kando na kuwafurusha wanachama ambao wanaegemea upande mwingine, pia watajadili njia ya kubuni mrengo wa kisiasa na vyama vingine.

Baada ya kususia mkutano wa Mei 11 katika Ikulu, Wakenya wengi wana hamu ya kutambua endapo Ruto atahudhuria mkutano wa NMC na kisha mkutano wa Kundi la Bunge la Chama cha Jubilee ambao umeratibiwa kuandalia Juni 2.

Aidha imeibuka kuwa sehemu ya wandani wa Naibu Rais huenda watapuuza mkutano huo endapo wataalikwa.

Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa alisema alipata fununu kuwa kuna njama ya kutoalikwa lakini kama wandani wa Ruto watahudhuria hata bila ya kualikwa.

4. The Standard

Kando na hofu, huenda Ruto ataendesha siasa za kulipiza kisasi endapo atachukua hatamu za uongozi 2022, The Standard limejaribu kuelezea sababu za Ruto kuhofiwa na watesi wake.

Kiongozi wa Wachache Bunge la Taifa, John Mbadi alisema Ruto amejigeuza kuwa safu ya kushambuliwa kwa sababu ya uongozi wake duni.

Mbadi alimkashifu Ruto kwa kufanya azma yake ya kuwania urais kuonekana kama hatari nchini.

Gavana wa Machakos, Alfred Mutua na Mbunge wa Nyeri Town, Ngunjiri Wambugu walisema madai ya ufisadi yanayomzingira Naibu Rais yamewachochea wengi kumpinga kwani tuhuma hizo zinachora taswira ya uongozi wake endapo ataingia Ikulu.

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa na Seneta wa Nandi, Samson Charargei wanadai Ruto anashambuliwa kwa sababu ana ushawishi mkubwa na mahasimu wake wanafanya kila jitihada kumzuia kumrithi Uhuru.

Wachanganuzi wa siasa Herman Manyora na Edwin Kisiangani wametambua kwamba shambulizi dhidi ya Ruto ni ishara kwamba ni tishio kwa wagombeaji wengine wa urais nchini.

5. Daily Nation

Gazeti hili linaripoti kuhusu kisa cha kushangaza ambapo watu waovu wamegeukia kuharibu makaburi ya Lang'ata kujichumia mapato.

Watu hao wasiojulikana huchimbua makaburi wakati wa usiku wa manane ambapo hung'oa vyuma vilivyowekwa na waombolezaji kuboresha makaburi ya wapendwa wao.

Kando na kupamba makaburi hayo na vyuma, watu hao hutumia msingi thabiti kuwazuia wezi wa majeneza.

Gazeti hili linaripoti kuwa baada ya wezi hao kuiba vyuma, huwauzia wafanyabiashara wa vyuma kujipatia mapato.

Kwa hivyo endapo ulimzika mpendwa wako katika makaburi ya Langata na kuimarisha kwa vyuma, utahitajika kwenda kuthibitisha ikiwa bado ni salama.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaoZxfJBmpJqfka%2BytbWMsphmoqWirq%2B6xGaknqFdZ4NuucCcn6hlqaTBpnnKsJhmnKBiv7bAzmaumqORqbZuw8BmpKStpJa7sHnWmmSuoKWnwm61yq6jrmaYqbqt