Kisumu: Watahiniwa 2 wa KCPE wajifungua dakika chache kabla ya kuanza kufanya mtihani

Publish date: 2024-09-03

Watahiniwa wawili wa mtihani wa kitaifa KCPE mwaka huu kaunti ya Kisumu wameripotiwa kujifungua dakika chache kabla ya mtihani wa kitaifa kuanza Jumanne, Oktoba 29

Mmoja wa watahiniwa hao alijifungua katika hospitali ya kaunti ya Ahero na yuko katika hali nzuri kulingalina na taarifa za runinga ya Citizen.

Habari Nyingine: Wakandarasi wa China waliokuwa wameleta uzembe TZ waanza kazi baada ya kunyoroshwa

Taarifa za The Standard ziliarifu kuwa takribani watahiniwa wanne kutoka kaunti ya Narok, Bomet na Nakuru wanafanyia mtihani wao katika hospitali tofauti.

Wanne hao wanasemekana kujifungua saa chache kabla ya kuanza kufanya mtihani wao Jumanne, Oktoba 29.

Habari Nyingine: Familia ya Mzee Moi yakana madai kuwa yuko katika hali mbaya

Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE ulianza rasmi Jumanne, Oktoba 29 ambapo zaidi ya watahiniwa milioni moja walijisajili kuufanya mtihani huo mwaka huu.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ354fpZmoqKrpaLCbsPArZihoZ6exKJ5kWaummWbmL2medaaoaKepaO0tq2MnZikoZuWeqS0wJyfnmWblq%2BtrYyymGajpZa7u62MpKyfmZ6urm6506KfmqaZY7W1ucs%3D