Njia 17 za kusisimua maisha yako ya mapenzi baada ya kujifungua

Publish date: 2024-07-07

Watoto huja na baraka kwa familia, kando na kuwatwika wazazi, hasa wanawake majukumu ya kuwalea na kuendeleza majukumu mengine ya maisha kama ya kikazi.

Baada ya kujifungua, wanawake wengi hupoteza hamu ya mahaba kwa kiwango cha kutowataka wapenzi wao kuwagusa.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Mwanamke amshataki mpenziwe kwa kumuuma sehemu nyeti kitandani

Habari Nyingine: Afisa wa trafiki acheza densi barabarani, asahau habari ya hongo (video)

Kutokana na maumivu ya mwili na hisia ya kutovutiwa na mumeo, wanawake wengi hukosa kuvutiwa na mialiko ya wapenzi wao kuwa na muda wa mapenzi kati yao.

Hata hivyo, hali haistahili kuwa hivyo. Maisha yako ya mapenzi inaweza kuimarishwa na kurejelea hali yake ya kawaida.

Habari Nyingine: 80% ya mutura zinazouzwa Nairobi zina uchafu unaosababisha magonjwa - utafiti

Wazia suala hilo kama kuunganika kwako na mpenzi wako na sio tu kula uroda.

Pia usiwe na matarajio mengi, uwe mtulivu na kuelewa kuwa mahaba yanaandaliwa.

Habari Nyingine: Mtoto wa nyoka ni nyoka; bintiye Akothee ajianika nusu uchi

TUKO.co.ke imekuorodheshea mbinu ambazo unaweza kutumia kurejesha mapenzi kati yako na mpenzi wako baada ya kujifungua:

1.Wazia kushiriki mapenzi na mpenzio kama njia ya kuondoa uzito wa kutatizika kwa akili na mambo yanayokutatiza.

2.Elewa kushiriki mapenzi kama njia ya kuunganika na mpenzio na sio tu kula uroda.

3.Ikiwa mambo sio mazuri kwenye chungu la asali kwa sababu ya ukavu, usisite kutumia mafuta ya ulainishaji.

4.Tumia mwangaz isiyo kali kwenye chumba cha kulala na mshumaa yenye harufu nzuri na inayoeza kuzingua kuimarisha hamu ya mahaba.

5.Nunua nguo za ndani zinazomvutia mpenzio na kunasa hisia zake.

6.Usiweke ratiba ya kufanya ngono nyakati za usiku tu, jaribu kutafuta uroda hata mchana.

7.Jiunge na mumeo kwenye bafu na kujaribu kupakuliana mahaba humo.

8.Usiosope kumuonyesha mumeo kwa watu.

9.Waandae watoto walale mapema ili wewe na mpenzio mpate wakati wenu.

10.Kuwa mtundu kwa mahaba na kushiriki ngono ya haraka.

11.Kujiepusha na kuchoka nyakati za usiku, lala mchana ili uwe na nguvu nyakati za usiku kupakua mahaba.

12.Jijali na ujishughulikie wakati mumeo hayuko nyumbani na uwe na muda wako bila yeye kuwepo. Kukosa kuwepo kwake kumaufanya moyo kumtamani.

13.Waombe jamaa na mafariki wawaangalie watoto na ukahifadhi chumba cha hoteli kwa usiku mmoja.

14.Andaa mikutano ya mahaba nyakati za usiku.

15.Mpigie mumeo na umzingui kupitia kwa simu ili awe na mawazo na kutarajia vitu vizuri kutoka kwako.

16.Kubali udhaifu wa mwili wako na kufurahia ngozi ya mwili wako.

17.Kitanda kiwe chako na cha mume wako. Waache watoto walale kwenye vitanda vyao.

Read ENGLISH VERSION

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Hii ndio sababu ya Jacque Maribe kuachiliwa kwa dhamana | TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdibn5xfpZmpaOhkWJ%2BeHnZmmSkraOewKq51JpkppmZqLWiediaoqhlqZZ6rq3PnqWzoV2XrqKwwGawmmWbqreqstSnnq6ZXp3Brrg%3D