Mpende msipende ushuru wa 16% ni lazima mtalipa Moses Kuria
- Kuria alisema, kutekelezwa kwa 16% VAT unaotozwa bidhaa za mafuta hakuwezi kusababisha bei ya bidaa zote kupanda na kwamba Wakenya ni sharti kulipa ushuru huo ikiwa wanataka Kenya kukua kiuchumi
- Wabunge walipitisha bungeni kuwa, utekelezaji wa ushuru huo ucheleweshwe kwa mudawa miaka miwili
- Uhuru anatazamiwa kutia saini mswada huo lakini ikiwa hatautia saini, Wakenya watalazimika kuendelea kushuhudia bei ya juu ya mafuta
Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria, amesema Wakenya ni sharti kulipa ushuru wa thamani (VAT) wa 16% na kwamba wanaopinga sio wazalendo.
Kulingana na Kuria, kulipa ushuru ndio njiaya pekee ya kuhakikisha Kenya inakua kimaendeleo na kiuchumi.
Habari Nyingine : Mzee amchemkia mwanawe kwa kupenda 'masponsa'
Aakizungumza kupitia Citizen TV Jumanne, Septemba 11, mbunge huyo alisema, bei za bidhaa haziwezi kupanda kwa sababu ya ushuru huo.
"Hamna VAT katika unga wa mahindi. Bidhaa za msingi hazitozwi. Hata kama VAT itatekelezwa katika bidhaa za mafuta, bidhaa za msingi zitabakia zilivyo," alisema.
Habari Nyingine : Picha 11 zinazoonyesha maisha ya kifahari aliyokuwa akiishi Sharon Otieno kabla ya kuuawa
Kuria alionekana kuwa na ufahamu mkubwa kuhusu Rais Uhuru Kenyatta kukataa kutia saini mswada huo wa 16% VAT ambao wabunge walitaka usitishwe kwa muda wa miaka miwili.
"Tutalipa VAT kwenye bidhaa za mafuta. Niamini. Kwangu ushuru ni muhimu na ninaamini kulipa ushuru ni kujitegemea. Aliyekuwa rais Mwai Kibaki alitufundisha," alisema.
Habari Nyingine : Sharon Otieno siye wa kwanza; mabinti wengine 4 waliofariki baada ya kujihusisha na watu mashuhuri
Tangu kupitishwa kwa mswada huo bungeni na Uhuru hajatia saini, Waziri wa Fedha, Henry Rotich, aliamrisha utekelezaji wa ushuru huo kuanza Septemba 1, 2018.
Kutekelezwa kwa ushuru huo kumesababisha bei ya bidhaa za mafuta kupanda na hatimaye bidhaa za msingi.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine : Huyu ndiye mrembo aliyeivuruga ndoa ya Ababu Namwamba?
Juhudi za Mahakama ya Juu mjini Bungoma kuamrisha ushuru wa 16% VAT usitekelezwe bado amri hiyo haifanyi kazi huku lita moja ya mafuta ya petrol ikiuzwa kwa KSh 127.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYJ4f5JmpKmdnpmybrnSoqeeppSaera%2Fx66prmWnlnpygoynoGakka%2B2rq2MpquapJmlrm65zqycrGWbqr%2BqrY2hq6ak