Wasanii wa muziki Uganda wamwandikia barua Museveni, wamtaka amwachilie huru Bobi Wine
- Wasanii wa muziki nchini Uganda wameungana kwa pamoja mitandaoni kumshawishi Rais Yoweri Museveni kumuachilia huru mara moja Bobi Wine aliyekamatwa Jumatatu
- Jose Chameleone, Eddy Kenzo, Vinka, Weasel, Juliana Kanyomozi, Irene Ntale na watu wengine maarufu nchini humo, ni miongoni mwa wanaotaka Mbunge huyo wa upinzani wa jimbo la Kyadondo kuachiliwa huru
Kufuatia kukamatwa na kuendelea kuzuiliwa kwa Bobi Wine, wasanii wa muziki nchini Uganda wameungana kwa pamoja na kumtaka Rais Yoweri Museveni kumuachilia huru mara moja Mbunge huyo wa upinzani wa jimbo la Kyadondo.
Habari Nyingine : Ngina Kenyatta na mabinti weingine 9 wa marais wa Afrika wanaopendeza ajabu
Jose Chameleone, Eddy Kenzo, Vinka, Weasel, Juliana Kanyomozi, Irene Ntale na watu wengine maarufu nchini humo, wametumia mitandao ya kijamii kumshawishi Museveni kumwonea huruma Bobi Wine ambaye pia ni msanii na kumwachilia huru.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine : Mkenya Akuku Danger na wanaume 10 walioandikisha rekodi ya kuwa na watoto wengi zaidi duniani
Habari Nyingine : Brazameni aliyedai kulala na wabunge 13 aibuka tena na ujumbe mtamu kwa Sabina Chege
TUKO.co.ke iliripoti kuhusu polisi kumkamata Wine mjini Arua siku ya Jumatatu, Agosti 13, kwa kudaiwa kuchochea ghasia na kusababisha wafuasi wake kuvamia msafara wa Museveni.
Museveni alikuwa pia kwenye kampeni mjini humo wakati Wine na wenzake kutoka Upinzani walipokuwa wakimpigia kampeini mwaniaji huru.
Habari Nyingine : Mjukuu wa rais mstaafu Daniel Moi awazuzua wasichana mtandaoni
Ripoti kutoka nchini humo zinasema kuwa, Wine atasalia rumande kwa wiki moja ijayo na hii ni baada ya kufunguliwa mashtaka ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria na uhaini ambao hukumu yake ni kifo.
Hata hivyo, kaka yake mwanamuziki huyo amedai kama familia hadi sasa hawajui yuko wapi ingawa polisi nchini humo wamedai kuwa amelazwa hospitalini na anapokea matibabu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYByfZRmrpqrkaO2qnnWmmSmraqeuKp51KCYp5yRYsSiudaapZ2hm56ubq7Aq6yaZZ2qwKbCxKegZq%2BRosGit8BmmKavkZi1qrjInmShraKqeqO7waJksKGemnupwMyl