Mchezaji maarufu wa Harambee Stars, Rishadi Shedu aomba msaada kwa wahisani
-Rishadi Shedu alikuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa Harambee Stars wakati wake
-Amekuwa akiuguza jeraha mbaya la kiwiko ambalo linahitaji upasuaji nje ya nchi
-Gharama ya upasuaji huo ni KSh 1.8 milioni na anaomba msaada kutoka kwa wahisani wema
-Mchezo wa kandanda haungekuwa ulipo haingekuwa kujitolea kwake na wengine wakati wake
Rishadi Shedu, alikuwa mmoja wa kocha maarufu zaidi wa kandanda eneo la Afrika Mashariki.
Habari Nyingine: Chiloba akumbana na vijana wenye ghadhabu kaunti ya Trans Nzoia
Aliacha kucheza 1985, baada ya kupata jeraha la goti ambalo lilimzuia kucheza kabisa.
Straika huyo wa Harambee Stars wa zamani, hivyo aliamua kuwa kocha, ili kutoa mafunzo kwa wachezaji. Akiwa meneja, alipata jeraha la kiwiko alipokuwa katika klabu ya Bandari.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Alipata jeraha hilo kutokana na kuwa uwanja walimokuwa wakichezea uliokuwa na shimo ambalo halikuwa likionekana.
Machi 2016, aliamua kuacha kutoa mafunzo ili kuuguza mguu wake. Katika mahojiano na KTN, mchezaji huyo shupavu alisema ulingo wa kandanda nchini ulikuwa umemtelekeza na kuongeza kuwa lilikuwa jambo la kuvunja moyo ikizingatiwa kuwa alijitoa sana katika kazi yake.
Habari Nyingine: Rais Museveni asema kwa nini hajanywa soda tangu 1965
"Wakati wangu, wachezaji walicheza bila mshahara, tulicheza kwa kuipenda nchi,” alisema Shedu.
Mguu wake ulioumia vibaya ulimlazimisha kukoma kutoa mafunzo kwa timu kubwa. Jeraha hilo linamhitaji kusafiri nje ya nchi kupokea matibabu maalum.
Habari Nyingine: Muimbaji Jose Chameleon aoyesha mashabiki gari lake jipya la KSh24 milioni
Gharama ya matibabu hayo inakadiriwa kuwa KSh1.8 milioni, na anaomba msaada wa wahisani wema.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4J2gJhmpJygla%2Buq7WMppiaqqWbwm7DwGafmqqRoq%2BmsYysq5qqo2K%2Fqr%2FHmpuiZaOdsqXBjJqmppqRYrq0rcCdmGajp5Z6uK3HoqqappljtbW5yw%3D%3D