Ungefanya nini iwapo ungegundua mpenzi wako huwa haoshi vyombo vyake? Wanawake Wakenya wajibu

Publish date: 2024-07-14

Wanawake wengi huapa kwamba hawawezi kuishi na mwanamme mchafu asiyetilia maanani usafi wake.

Wengine husema endapo wapenzi wao ni wachafu, watajitolea kushughulikia chochote kinachohusu usafishaji.

Hata hivyo, ni rahisi kusema haya kuliko kutenda maadamu watu hutoroka pindi wanapokumbana na jamaa asiyejali na mchafu.

Habari Nyingine: Kutana na mwanamke mrembo Mkorino anayewakosesha wanaume usingizi

Hebu fikiria, mpenzi wako anakualika kwake adhuhuri moja. Unaingia jikoni mwake na unapata mlima wa vyombo vichafu ambavyo vimekaa pale kwa wiki moja au hata zaidi.

Utatoroka au kuweka mkoba wako chini na kuanza kusafisha vyombo?

TUKO.co.ke iliwauliza wanwake Wakenya swali hilo na baadhi ya majibu yao ni ya kushangaza.

Humtoz Young Gee Nitaketi na kuanza kucheza kibao cha Jenifer Lopez "I ain't your mama" kama yeye si ngiri, bila shaka ataelewa ninachomaanisha.

Habari Nyingine: Mwanamke aliyedaiwa kwa kulala na Raila Odinga aeleza bayana kilichtokea

Nancy Chrispar Mpenzi wangu anawajibika mno. Mimi huosha tu tunavyotumia wakati huo.

Faith K Kalungu Nitaondoka taratibu na kumwacha jamaa huyo maskini pekee yake.

Kamitah Hannah Mukuhi Nitaviosha kasha niviweke vyote katika kabati linalofungika na kuacha kikombe kimoja, kijiko, sufuria 2 na nibebe funguo.

Emmeldah Beryl Lakini tayari ulisema "mpenzi" weka kistari neno "mpenzi" au uliweke kwa herufi kubwa. Sitagusa hata kijiko.

Habari Nyingine: Je wanaume wanahitaji nini katika uhusiano? Wakenya watoa maoni yao

LovelyLucy Lither Nitaacha jikoni jinsi lilivyo. Usijali kuwa mke ilhali bado unamiliki cheo cha mpenzi.

Becky Adams Hilo ni suala kubwa? Nitaviosha, nimpe tunda afurahie ili asahau usumbufu wa vyombo vichafu jikoni mwake.

Mercy Kitaka Mimi huheshimu maamuzi ya watu..iwapo anaacha jikoni mwake hivyo, inaamanisha analipenda likiwa hivyo.

Habari Nyingine: Mcheshi Eric Omondi aonyesha ‘silaha’ yake na kuwaacha Wakenya vinywa wazi

Jackline Mackay Nitamtumia ujumbe dadangu na kumwomba anipigie haraka kasha simu yangu ikilia nitaichukua na kuanza kulia kwamba dadangu amelazwa hospitalini, nikishaondoka hatowahi kuniona hapo tena.

Shama Sp Hakuna lolote kati ya hayo. Mwanamke anapaswa kumnyorosha jamaa huyo aoshe vyombo hivyo mara moja!! Hafai kuosha vyombo ambavyo hakuvitumia.

Kendi Kimathi Eeeeish, huo ndio mwisho, ni vigumu kuishi na wanaume kama hao katika siku za usoni.. Nitamtilia maanani tu iwapo ni mtu alie nadhifu.!

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4F4fZBmrKeflZuur8XAZqWipplitritz6hkrqaXmrS2usOumGaloJq7u7WMsJikp12dwritjKGYqKuYnnq3xc6mmahlpq6urLGMsJinmaeWuKZ51pqinqaplnq4rcmima5mmKm6rQ%3D%3D