Mbunge wa Jubilee aandamwa na madai ya UNYAKUZI wa ardhi
- Julius Ndegwa Kariuki atafikishwa mahakamani Jumatatu Machi 13 kwa kughushi sahihi ya marehemu kuiba shamba
- Alisemekana kulipa kwa kipande hicho cha ardhi mara sita lakini kwa kutumia cheki ghushi
Habari Nyingine: Mercy Masika awasisimua Wakenya kwa picha ya KUPENDEZA ya bwanake na watoto
Mbinge wa Lamu Magharibi Julius Ndegwa Kariuki anatarajiwa kufika mahakamani Mombasa kwa kughushi sahihi ya marehemu kuiba shamba.
Julius Ndegwa Kariuki anasemekana kughushi marehemu Omar Kola Barisa ili kujipa shamba lake la hektari 4.5 eneo la Hindu, Kaunti ya Lamu.
Pata HAPA habari za TUKO.co.ke punde tu zinapochapishwa!
Mbunge huyo anatarajiwa kufika mahakamani Machi 13, 2017.
Ndegwa anashutumiwa kwa kudanganya kwa kutumia cheti ghushi kuuza kipande cha ardhi kisicho chake kwa wafanyibiashara Yussuf Sufi Abasheikh na Mohaddin Abasheikh kwa KSh.4, 000,000 mwaka wa 2013.
Habari Nyingine: Mwanamume akamatwa baada ya kujifanya mwanamke kwa HARUSI (picha)
Anasemekana pia kulipa kipande hicho kwa kutumia hundi akijua akaunti yake haikuwa na pesa mara sita baada ya kuuziwa tena kipande hicho mwaka wa 2012.
Jaji Dorah Chepkwony Ijumaa Machi 10 aliagiza kushtakiwa kwa mshukiwa huyo katika Mahakama ya Mombasa baada ya kufutilia mbali dhamana ya KSh 500,000 na mdhamini wa kiasi hicho alichokuwa amepewa na mahakama Jumatano Machi 8.
Habari Nyingine: Mwanamume amlipa rafiki yake MSHAHARA ili amtunge mimba mke wake; kinachofuata kinashangaza
Ndegwa na wanachama wa kamati ya CDF Eneo Bunge la Lamu Magharibi wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya mamlaka mwaka wa 2015 kulingana na Baraka FM.
Subscribe to watch new videosRead ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: aron.mtunji@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaIB1hJNmpJutnpyybsPAZqGumpmhsqZ5wJqlnZmdrK5uusBmpJqckZ56uq2MrqWymZuqx6p51ppkmqqUnbZvtNOmow%3D%3D